Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Saturday, August 9, 2014

Asubuhi ya leo Kibonde wa Clouds anadaiwa
kusababisha ajali asubuhi hii eneo la
Makumbusho, amemgonga dereva mwingine
kwa nyuma. Trafiki walipofika kupima ajali,
Kibonde karudi nyuma kaendesha gari lake
kasepa! Trafiki katumia gari lililogongwa
kumfukuzia. Walifanikiwa kumkamata eneo
la Mwenge. Trafiki aliingia katika gari lake
nakumwomba arudi eneo la ajali ili
wakapime na kuchora mchoro wa ajali.
Kibonde kagoma na kumtaka trafiki ashuke
katika gari lake, trafiki naye kagoma
kushuka. Mchezo ulioendelea Kibonde
aliondoa gari na kuanza kupiga misele,
akizunguka mitaa akiwa na trafiki huyo!
Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao
walianza kuifuatilia gari hiyo ya Kibonde kila
kiunga cha jiji hususani eneo la Mwenge na
Ubungo. Hayawi, hayawi yakawa, Kibonde
akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo,
hapo nikashuhudia senema ya Kibonde na
trafiki! Trafiki wa kike aliyekua eneo hilo
akaipiga mkono gari ya Kibonde iliyokuwa
kasi, gari hiyo haikuonesha dalili za
kupunguza mwendo. Trafiki alikomaa
kusimama mkono wake ukiwa juu kuashiria
kumtaka Kibonde asimame huku akipaza
sauti katika radio call akisema ananigonga,
afande, ananigonga! Akiwa katika hali hiyo,
kuna gari ilikotokea sikujua ikakatisha kati
ya trafiki na gari ya Kibonde ndiyo ikawa
kigingi cha gari ya Kibonde na kutiwa
mbaroni na Kupigwa Mitama kadhaa
Aligoma kuendesha gari ikabidi livutwe hadi
polisi Urafiki ambapo kwa sasa amepelekwa
Oystabay! Kwa utafiti wangu kidogo
nilioufanya nikifukuzana na muda kuwahi
kanisani, ni kwamba Kibonde na watu
wengine aliokuwanao ndani ya gari lake
walikuwa 'TINGASI'!

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni