Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Friday, August 15, 2014


Leo Diamond Aliamua Kuwajibu Mashabiki wa Wema Sepetu walio mshutumu
anamtumia Wema Kwa Faida yake
Bahati mbaya, majibu ya Diamond kupitia Instagram yamekuwa makali kiasi
cha kuwashtua wengi na kuona kama kamkosea heshima mpenzi wake.
Kwakuwa sitaki kuonekana kama namhukumu Diamond kwa kile
alichoandika, ningependa kuongea kwa lugha ya busara kadri iwezekanavyo,
na isitoshe nimegusia suala la ‘udhaifu’ na ‘ubinadamu’ katika aya zangu za
mwanzo.
Diamond ametumia kauli nzito na ya hasira kidogo katika kuwajibu vinara wa
kampeni hiyo. Si jambo la busara kumuita mtu umpendaye kwa kuandika
‘msanii wenu’ baada ya jina lake, pale alipoanza kwa kuandika: Nafikiri
ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa ‘Msanii wenu’.
Ingekuwa vyema kama angeandika; Nafikiri ningewaona kweli Mnaakili na
Mapenzi ya dhati kwa ‘Wema Sepetu’. Again, hizo ni hasira tu na ndio maana
aliamua kuifuta post hiyo Kwa maelezo aliyoyatoa staa huyo, imebainika wazi kuwa ni Wema ndiye
aliyeamua kuishi hivyo na pengine ameridhika na hatua aliyofikia.
Inavyoonekana Diamond hapendwezi na muenendo na maisha ya mpenzi
wake hasa kwa kudai anaendekeza urafiki na watu wanaopenda anasa na
kula bata.
“Mngemshauri apunguze mashoga wapenda anasa na apunguze starehe
zisizo na faida, wenda ingemsaidia pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na
kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe,” yanaendelea
kusomeka majibu ya Diamond. Maelezo hayo yanaeleweka wazi kuwa Wema
amekuwa ni mtu wa starehe na kula raha na marafiki zake (Aunty Ezekiel
haikwepi hii sentensi, inamhusu). Kwa kauli ya Diamond, Wema anaonekana
kuendekeza ulevi kwa kutumia fedha anayopewa na mchumba wake.
“Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha mpenzi wangu anakula
vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumwezesha mtaji wa kufanyia kazi.”
Sentesi hiyo inamaanisha kuwa, Diamond anatimiza wajibu wake na tayari
amempa mtaji mpenzi wake. Kuna taarifa pia kuwa hata filamu yake ya Family
aliyoigiza na Aunty Ezekiel ilidhaminiwa na Diamond.
“Waswahili wanasema mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka
ng’ombe wake kwenye maji safi, ila yeye ng’ombe mwenyewe ndio
anatakiwa aamue kunywa maji,” anaendelea Diamond. “Au mnataka
nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ?
Nisiende studio nikae dukani nimuuzie mie? Ni juhudi zako kwanza.”
Maneno ya Diamond yanajielezea yenyewe kuwa Wema amejisahau. Maswali
ya wengi ni kuwa wao kama wapenzi hawajawahi kuzungumza haya na
kushauriana? Diamond hajawahi kumkanya mpenzi wake kuwa mwenendo
wake sio? Au ameshamuambia hadi amechoka na ndio maana ameamua
kuuambia umma kile kinachoendelea?
Kwa lawama na matusi ambayo Diamond ameyapata kutokana na kampeni
hiyo, ilikuwa inahitaji uvumilivu wa hali ya juu kukaa kimya. Nahisi uvumilivu
ulimshinda na ndio maana aliamua kuandika alichokiandika ambacho bahati
mbaya kinaweza kutia tena doa uhusiano wao. Sijui Wema atasemaje!!

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni