Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Thursday, August 7, 2014

Stori:Mayasa Mariwata
KAULI ya nyota wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwamba hawezi
kuoa kamwe, inadaiwa kumchefua
mwandani wake, Wema Isaac Sepetu
‘Beautiful Onyinye’, Amani limenyetishiwa.
Aliporejea Bongo kutoka Marekani juzikati,
Diamond alitoa kauli hiyo na kuandikwa
kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti dada
la hili, Ijumaa, toleo la wiki iliyopita likiwa na
kichwa cha habari; ‘DIAMOND: SITAOA
KAMWE’ ambapo ndani yake alieleza jinsi
ambavyo mastaa wengi waliooa
wameanguka kisanii.
MTU WA KARIBU AYASEMA YA WEMA
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa
hao, Wema hakufurahishwa na habari hiyo
kwa sababu anajua yeye ndiye mke
mtarajiwa wa Diamond.
Ilidaiwa kwamba, Wema alijikuta akipoteza
ile furaha ya kwamba wawili hao
wangefunga ndoa mwezi huu (Agosti) kama
ilivyotabiriwa na mnajimu maarufu Bongo,
Maalim Hassan Yahya Hussein.
“Baada ya kauli hiyo ya Diamond na
kutotimia kwa utabiri wa Maalim Hassan
kwa sababu hakuna hata dalili za maandalizi
ya tukio hilo muhimu kwenye maisha ya
mwanadamu, Wema ameanza kukata
tamaa, lakini amesema hawezi kulazimisha
ndoa kwa mwanaume kwa kuwa si
utamaduni wa wanawake wa Kitanzania
wala Kiafrika.
“Unajua Kibongobongo au hata Kiafrika hai-
sound vizuri na pengine haiwezekani kwa
mwanamke kulazimisha kuolewa kama
mwanaume hataki. Hicho ndicho
kilichomtibua Madam (Wema) baada ya
kusoma alichokisema Diamond,” kilisema
chanzo hicho na kuongeza:
“Wema amehisi yeye ni girl lover (mpenzi)
tu kwa Diamond na si wife material (mke
mwema) kwa hiyo anawaza sana kuhusiana
na ishu hiyo japo mahaba niue kati yao
yanaendelea, lakini anafikiria kuchukua
uamuzi mzito.”
WEMA SASA
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, gazeti hili
lilimtafuta mlimbwende huyo anayeshikilia
Krauni ya Miss Tanzania 2006 ili kumsikia
mwenyewe ambapo alifunguka yake ya
moyoni.
Mwanadada huyo alisema kuwa kwa sasa
haumizi tena kichwa kuhusu suala la ndoa
na Diamond na kwamba hana haraka nalo.
“Mimi naamini sana mambo ya utabiri,
lakini siumizi kichwa na suala la kuolewa na
Diamond na kamwe siwezi kumlazimisha
anioe.
Aliporejea Bongo kutoka Marekani juzikati,
Diamond alitoa kauli hiyo na kuandikwa
kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti dada
la hili, Ijumaa, toleo la wiki iliyopita likiwa na
kichwa cha habari; ‘DIAMOND: SITAOA
KAMWE’ ambapo ndani yake alieleza jinsi
ambavyo mastaa wengi waliooa
wameanguka kisanii.
MTU WA KARIBU AYASEMA YA WEMA
Kwa mujibu wa mtu wa karibu wa mastaa
hao, Wema hakufurahishwa na habari hiyo
kwa sababu anajua yeye ndiye mke
mtarajiwa wa Diamond.
Ilidaiwa kwamba, Wema alijikuta akipoteza
ile furaha ya kwamba wawili hao
wangefunga ndoa mwezi huu (Agosti) kama
ilivyotabiriwa na mnajimu maarufu Bongo,
Maalim Hassan Yahya Hussein.
“Baada ya kauli hiyo ya Diamond na
kutotimia kwa utabiri wa Maalim Hassan
kwa sababu hakuna hata dalili za maandalizi
ya tukio hilo muhimu kwenye maisha ya
mwanadamu, Wema ameanza kukata
tamaa, lakini amesema hawezi kulazimisha
ndoa kwa mwanaume kwa kuwa si
utamaduni wa wanawake wa Kitanzania
wala Kiafrika.
“Kikubwa katika mapenzi ni upendo wa
kweli ambao ananionesha bila kipimo. Wala
sina papara, hata kama mtabiri kasema
ndoa yetu ni lazima ifungwe mwaka
unaogawanyika kwa mbili kwa maana ya
mwaka 2016 kama itashindikana mwezi
huu, hilo kwangu si tatizo la kunifanya nililie
kuolewa na Chibu (Diamond).
“Ninachojua mimi Mungu ndiye anapanga
yote na kama ndoa ipo ipo tu maana kuna
watu wapo kwenye ndoa na hawana
upendo wa kweli kama tulionano sisi,”
alisema Wema.
MAMA WEMA ANASEMAJE?
Paparazi wetu alimtwangia simu mama yake
Wema, Mariam Sepetu na kumuuliza
mambo mawili, kuhusu bintiye kuvishwa
pete ya ndoa na Diamond na suala la
Mbongo Fleva huyo kusema hataoa kamwe!
“Mimi niseme nini? Sina la kusema kuhusu
Wema. Mambo yake ni yake mwenyewe na
huyo Diamond wake. Kwanza kwa nini
mnipigie mimi, si mumtafute yeye
mwenyewe?” alisema mama huyo kwa sauti
ya utulivu.
MAMA DIAMOND AFUATA NYAYO
Katika hali ya kushangaza, mama Diamond,
Sanura Kasim ‘Sandra’ ameonekana kunawa
mikono kwa kauli aliyowahi kuitoa siku za
nyuma kuhusu mtoto wake na masuala ya
kutooa au kuoa.
Nasibu ni mtu mzima sasa, siwezi
kumpangia lolote kuhusu kuoa au kutooa.
Wakati ukifika, anaweza kusema lolote
ambalo ataliona ni zuri katika maisha yake.”
KUHUSU PETE YA NDOA
Kuhusu Diamond kumvisha pete ya ndoa
Wema, tendo ambalo lilifanyika hivi karibuni
wakiwa nchini Afrika Kusini, Amani
lilifanikiwa kuzungumza na shehe mmoja
ambaye aliomba hifadhi ya jina lake
ambapo alisema alichokifanya Diamond kwa
Wema ni usanii.
“Diamond amemfanyia usanii mwenzake.
Pete gani bila kufunga ndoa. Halafu katika
Uislam, hakuna tendo la wanandoa
kuvalishana pete, hayo mambo
wanayafanya wenyewe, ” alisema shehe
huyo.
WEMA AIZUNGUMZIA PETE
Wema alipopewa nafasi ya kuizungumzia
pete hiyo alisema Diamond aliipenda tu
akaamua kumnunulia na kumvisha lakini
haihusiani na ndoa.
“Sisi (na Diamond) tulikuwa Afrika Kusini,
baby wangu akaipenda pete, akainunua na
kunivalisha, haina uhusiano na ndoa,”
alisema Wema.
GPL

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni