Kuna wanawake sijui wanafikiria vipi maisha.
Nilikuwa na girlfriend ambaye tulidumu karibia miaka minne, tulikua tunaenda vizuri na mipango mingi, ila akaanza kubadilika alivyokaribia kumaliza chuo, akawa na visa vingi na kuanza kuwa na marafiki wa ajabu ajabu wa kiume.
Kuna siku alikuja kunitembelea wakati anaondoka nikataka nimsindikize lakini akawa anakataa, nikamwacha akaondoka lakini baada ya muda mfupi nikaelekea mwelekeo aliokwenda, nikakuta kuna gari inamsubiri ndani kunamshikaji wakaondoka.
Nikampigia simu akapinga lakini nilivyompa details za gari ilivyo akakubali lakini akajitetea ni mshikaji.
Baada ya ku-argue kidogo akazima simu akaja kunipigia kesho yake, kunipa taarifa kuwa yule ni mtu wake mpya na tuachane.
Sababu aliyotoa kipindi kile ni kwamba mimi ni MPOLE sana (mimi ni mtu mwenye introvert personality), kwa hiyo akadai amepata mtu aliyechangamka na mjanja.
Ni kama miaka mitatu na miezi nane imepita, na mimi nilitulia nikajipanga na sasa nipo mbali kidogo na bongo.
Ila sasa hivi kuna kama mwezi mmoja nashangaa mtu ambaye nilishamsahau ananitafuta kwa nguvu mno, nmekuwa nikipata msg zake whatsapp, facebook, viber, sms za kawaida na amekuwa mpaka anamtumia shangazi yake kunitafuta, imefikia mpaka sasa hivi ananitumia picha zake za utupu( enzi hizo nlikuwa namsifia ana umbo zuri).
Nimeandika huu uzi sio kuomba ushauri, maana maamuzi ninayo japo na usenior bachelor wangu sirudi nyuma, ila ni kuwambia mademu hasa wadogo ambao mpo hapa ukiwa kwenye relationship, uwe mvumilivu na uangalie mambo kwa jicho la tatu, maana unamkimbia mtu kwa sababu ni mpole hana swaga. Lakini baadae (unaona 30 inakaribia bila bila) unarudi tena kwa kujidhalilisha na kutuma picha za uchi na kujitetea ulikuwa utoto ni noma mbaya.
0 comments:
Post a Comment