UREMBO! Mwigizaji wa sinema za Kibongo, Aisha Bui anahaha huku na kule kusaka dawa ya kuondoa makovu yaliyotokea katika baadhi ya maeneo ya mwili wake.Akizungumza na mwandishi wetu, Aisha alisema makovu hayo aliyapata hivi karibuni alipokuwa akicheza sinema iliyomtaka agalegale chini porini.
“Unajua filamu ni kitu ambacho kipo moyoni na nilitaka kuonyesha uhalisia wa ninachokifanya ndiyo maana sikuona shida kucheza huku nikigalagala kwenye nyasi, wakati mwingine siamini nilichokifanya ndani ya filamu hiyo ya Mshale wa Kifo inayotoka Jumatatu ijayo (leo),” alisema Aisha Bui.
0 comments:
Post a Comment