1. Huwezi kuwapenda watu wa nje kama huna mapenzi ya dhati kwayule uliyenaye kwenye uhusiano sasa.
2. Kumsaliti mwezio kwa kisingizio cha kulipiza kisasi huwa njia rahisi ya kukuingiza katika mgogoro binafsi na mwishowe kukuharibia kila mipango yako.
3. Kamwe usijidanganye kuwa utaweza kumsaliti na kumdanganya mwenzio kwa muda mrefu bila kugundulika, kila usaliti ni sawa na mimba lazima kuna muda utafika kila mtu ataiona tu.
4. Mahusiano yoyote hujengwa na uaminifu na kuthaminiana huku neno samahani na nimekusamehe likiwa nguzo kwa utatuzi wa kila tatizo mbele yenu.
5. Kusema nisamehe sio kuonekana mjinga bali pia huweza kukupa heshima na kuongeza mapenzi ya dhati baina ya yenu.
6. Neno nitakuacha au tuachane isiwe silaha ya kumwonea mwenzio maana nalo likizoeleka huweza kumfanya mwenza wako kuchukua maamuzi magumu kwani huashiria wewe una watu huko nje wakupao kiburi.
7. Kamwe usiwe mwepesi wa kuamini nini watu wanasema ila mshirikishe mwenzio kila uvumi ukoonyesha kumwamini na kumpa nafasi ya kukupa ufafanuzi.
8. Kila mahusiano huja na Baraka zake na huondoka na Baraka zake, unaweza ona unapata mafanikio sasa kwa sababu ya kuwa na huyo uliyenaye. Hivyo jitahidi kuzitazama kwa makini kila fursa njema upatazo na ona je zikiondoka utakuaje.
9. Fedha huleta ufahari lakini kamwe haina mchango katika kuleta furaha kwenye mahusiano yenu, hivyo pendaneni kama vile ni matajiri na maskini, kwani fedha yaweza kupotea muda wowote na kama mnapendana itarudi pia kwa kushirikishana jinsi ya kuirudisha lakini mapenzi yakiisha hata uwe na gunia la pesa ni kazi bure sawa na kuirudisha ladha ya chumvi siku ikiisha.
10. Mahusiano ya wawili hupendeza kama hayataingiliwa na watu wengine nanyi mkishirikishana katika kutatua matatizo na kuwa na maamuzi ya pamoja kwa kila jambo.
11. Ni vyema kutengeneza mazoea ya kujivunia na kuona ufahari kwa huyo uliyenaye na kama ukishindwa kuyafanya hayo kwa huyu hata ukimpata mpya mchezo utakuwa huo huo kwani bado huna ujuzi wa kuishi na mwenzako.
12. Huitaji kuwa dikteta kwa kuwa na misimamo ya kikoloni bila ya kuwa na utambuzi wa kuwa mko watu wa wili hivyo acha tabia za ubinafsi.
13. Wanawake wazuri na wanaume wenye mvuto hawawezi kwisha amini uliyenaye hukumpata kwa bahati mbaya, mpende kwa dhati.
14. Kila maamuzi ufanyayo sasa ukiwa na stress au huna sress huwa na tabia ya kuihaibu kesho yako, hivyo jitahidi kuwa na subira katika kila jambo.
15. Mapenzi hayaonyeshwi kwa kufungua zipu au kwa binti kupanua miguu tuu, mapenzi ni hisia, jinsi mnavyoishi, maelewano, ushirikiano na mambo mengine mengi.
16. Upendo hausubiri siku ya Valentine, kila siku ifanye kuwa siku ya valentine kwa mpenzi wako.
0 comments:
Post a Comment