Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Saturday, September 20, 2014

SERENGETI FIESTA IRINGA GUMZO LA MWAKA

Msanii mkongwe wa Bongo Fleva, Herry Samir 'Mr Blue' akitoa burudani kwa wakazi wa Iringa.
Mashabiki wakiendelea kuimba pamoja na Mr Blue.
Mtangazaji wa Clouds FM B12 akiwapagawisha mashabiki.
Msanii wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee akifanya yake katika steji ya Serengeti Fiesta Usiku wa kuamkia leo Iringa.
Vanessa Mdee na wacheza show wake wakiendelea kutoa burudani.
Mashabiki wakiendelea kucheza.
Mashabiki waliojitokeza katika Tamasha la Serengeti Fiesta 2014 Iringa.
TAMASHA la Serengeti Fiesta 2014, usiku wa kuakia leo ilikuwa ni gumzo la mwaka kwa wakazi wa pande hizo kutokana na kufurika katika shoo iliyofanyika ndani ya Uwanja wa Karume uliyopo mjini hapo ambapo kulikuwa na makamuzi kutoka kwa wasanii mbalimbali.
Tamasha hilo lilifunguliwa kwa wasanii wachanga kupanda jukaaani kama vile  K-Star,G-Luck, Edu Boy, Baraka na baadaye kete ikageuka kwa kumpandisha msanii anayetamba na kibao cha Basi Nenda, Mo Music ambaye alipagawisha uwanja mzima kabla ya kushuka na kuwapisha Makomandoo ambao pia walipiga shoo ya nguvu. Baadaye walipanda wakongwe kama vile Vanessa Mdee, Mr Blue,  Young Killer,  Linah, Ommy Dimpoz, God Zillah na Afande Sele.
Shoo ilikuwa ya shangwe mwanzo mwisho na iliendelea hivyo hadi alipopanda Juma Kassim Nature aliyefunga burudani hizo.
(PICHA ZOTE NA MUSA MATEJA/ IRINGA, GPL)

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni