Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Thursday, September 18, 2014

Khanga hizi zina maana gani?

Mbunifu wa mitindo na mpenzi wa vazi la khanga Missy Temeke (siye aliyeuliza swali)
Mpenzi na mshabiki wetu maarufu aishie Lamu nchini Kenya mara kadhaa ametutumia orodha ya majina ya Khanga za Mombasa zinazotamba sana nchini humo. Majina hayo tumekuwa tukiyachapisha katika ukurasa wa vichekesho kila tunapoyapata. Hata hivyo jana nimepokea barua pepe kutoka kwa dada mmoja ambae ametaka aelezwe maana ya misemo (majina) ya baadhi ya Khanga maarufu tulizozitaja kwenye blog yetu.

Aidha dada huyo ameomba pia asaidiwe kufahamishwa kwamba Khanga zenye maneno hayo zinavaliwa maeneo au wakati gani na kwa lengo lipi. Ametoa mfano kwamba Khanga iliyoandikwa "Kazi ya Mungu haina makosa" ina lengo la kumfariji mtu aliyepatwa na matatizo na hivyo inafaa sana kuvaliwa kwenye misiba au unapokwenda kumpa pole mtu aliyepatwa na janga fulani.

Amefafanua kuwa kwa kawaida sio akili, heshima wala ustaarabu kwa mwanamke kuvaa Khanga iliyoandikwa "Ndio ukome si ulikuwa unaringa" wakati wa kwenda kumpa pole mwanamke mwenzio aliyefiwa na mumewe au kupatwa na masahibu yoyote kwa sababu utaeleweka vibaya kwani lengo la khanga ni kufikisha ujumbe. Kwa msingi huo, huyu dada anataka kujua maana ya majina na sehemu ambazo khanga hizi zinafaa kuvaliwa.
  • , Mganga Mungu
  • . Utamaliza limao dhahabu haiwi almasi
  • . Sio hapo chini kidogo
  • . Raha ya dodo lisiwe dogo
  • . Hujui kuosha si ajabu kakutosa
  • . Huu mwili wako anza upendako
  • . Unkula huu
  • . Tanua paja mkwaju waja
  • . Ya juzi lakini huitunzi
  • . Hupewi bila kuomba
  •  .Kuku hujamjulia bata utamuweza?
  •  .Hima hima nikupe anachokunyima
  •  Wenzio twaoga wewe waroga
  • .Raha ya shavu liwe kavu

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni