HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Season 19
ILIPOISHIA JANA
Kwa upendo na kujifanya ni machakarikaji akauona mpira pembeni na kuanza kuyamwagilia maua kitendo kilichomliwaza sana na kuona ni burudani huku akimwona baba mkwe akitabasamu kufurahia kile kitendo mkwewe.
Mara mama mkwe akaja na kusimama mbele yake akiwa na uso wenye jazba na sekunde chache maji yalikatika wakati mwakibubu akiwa hajui nini afanye au kwambia mkwewe akashtuka kutoka uswingizini na kugundua alikuwa ameshakojoa kitandani na ule mpira alioushika alikuwa ni...........
ENDELEA
Mara mama mkwe akaja na kusimama mbele yake akiwa na uso wenye jazba na sekunde chache maji yalikatika wakati mwakibubu akiwa hajui nini afanye au kwambia mkwewe akashtuka kutoka uswingizini na kugundua alikuwa ameshakojoa kitandani na ule mpira alioushika alikuwa ni askari kanzu wa eneo la uwanda wa chini kusini mashariki.
Nilicheka kwa dakika kadhaa huku nikiunganisha na tukio langu ambalo sikutaka kumsimulia bwana Mwakibubu kwani angenicheka zaidi hivyo tukaishia kunywa pombe zetu na kusema ni ajali kazini.
Tuliendelea kuwepo pale kwa zaidi ya masaa kadhaa na nikaanza kuhisi kuwa hali yangu haikuwa safi kwani muda huo ilikuwa ni saa tano za usiku na pombe ilishaanza kunizidia. Hivyo nikaagana na bwana mwakibubu na kuanza safari ya kurudi nyumbani.
Nilifika nyumbani salama na kulipaki gari na kulala kabla ya kushtushwa na kitu kigumu chenye maumivu makali kikiupiga mwili wangu bila ya kupumzika . Ile nafumbua macho nilikutana na kofi moja zito lililonipeleka sakafuni na kuanza kupata fahamu kwa mbali.
Kuangalia vizuri kumbe nilikuwa chumba cha binti yetu wa kazi huku nikiwa na boxer tuu na mama pachu akinitandika huku binti wa kazi akiwa anatokwa na machozi na kwa mbali nikaona alama za vidole mashavuni mwake kuashiria alianza muda mrefu kupokea vipigo.
" Nimekusikia vizuri ukiwa unapaki gari na hujaingia chumbani kumbe huu ndio mchezo wako kuingia chumbani kwa binti wa kazi? Nae bila hata aibu ajifanya kuja kuniita, mnanitengenezea picha eeee?? sasa leo nimejua na nitawakomesha.
Yaani maumivu ya jana hayajaisha na leo umekuja na jingine tena na hili ndio balaa au nikutangaze eeeeh???? Jibu sema KANTANGAZE na uone moto wake" Alisisitiza mama pachu.
Muda wote huo sikuwa na la kusema zaidi ya kumshangaa na kusikilizia maumivu ambayo bado sikuyatambua ni ya kifaa gani kwani mara ya mwisho kukutana na maumivu haya ni siku ambayo tuliandamana chuoni kwetu kudai mikopo na kuishia kupata kipigo hevi kutoka kwa walinda amani.
Kumtazama mama pachu alikuwa mkononi kashika mwiko wa kupikia chakula cha mbwa huku akitaka kuendelea kunipiga nikamsihi na kumwambia "mama utaniua yaani hata dada msamehe mimi sijui niliingiaje humu ndani na tena umshukuru Mungu wako nimefika salama maana sijui hata nimefikaje humu ndani".Mama pachu aliniambia nilale sebuleni na kesi itaendelea asubuhi.
Asubuhi nilishtushwa na sauti ya mtu akilia kilio cha chini chini na kuniambia, "baba pachu usipoziacha pombe zitakuja kukufanyia jambo la aibu sana. Ona sasa kazini umesimamishwa na umekuwa na matukio ya kusikitisha hebu kumbuka hata tulivyokuwa kule matema??
Nafikiri ni muda muafaka kwa wewe kuachana na pombe au uzidi kuharibu mambo yako na kumbuka una familia inakutegemea"... aliongeza kusema mama pachu na kuanza akusafisha makochi niliyoyataapikia.
Aliniandalia maji nikangia kuoga na baada ya kupata supu nikaondoka nikiwa sijui wapi nataka kwenda kwani nilihitaji kukaa sehemu na kutafakari kwa undani juu ya mustakabali wa maisha yangu kwani tangu binti yule wa kwenye simu aanze kuniandama nimepoteza furaha, amani, ujasiri na hata kazi nimeharibu huku familia ikiwa hainielewi na jamii inizungukayo.
Nikiwa njiani akili ikanijia kama mimi jana niliondoka nikiwa vile na kusababaisha uharibifu wa mazingina na tena nimeumia sana yaani naingia chumba cha beki tatu????? Wallpaper yake ya in front mbovu na hata hakanukii na behind hata bright future hana yaani niliumia sana na kujiona ni mpuuzi wa mwisho.
Nikafika pale kwa bwana mwakibubu na kuukuta malango ukiwa umefungwa lakini dalili zikionesha kuna mtu yuko ndani kwani sauti ya mziki ilisikika kwa chini chini na kuanza kuugonga mlango kwa bidii zote.
Nilikaa pale mlangoni kwa zaidi ya dakika 15 bila dalili ya mtu kutokea na ni wakati huu nikaamua kuzunguka na kugonga dirishani ambapo bwana mwakibubu alikuja na kunifungulia mlango.
Mama yaangu!!!!!!! Mama yaangu!!!!!!! Mama yaangu!!!!!!! huwezi amini nilichokiona kwani uso wa bwana mwakibubu ulikuwa umevimba na sehemu ya juu ya jicho ikiwa imechanika na damu zikiwa zimeganda. Akanikaribisha ndani na kuanza kunisimulia mkasa uliomkuta.
Akaanza kwa kusema, "Kaka jana baada ya wewe kuniacha pale niliendelea kupata bia kadhaa, sasa wakati najipanga kuondoka kuna simu iliita na mimi kwa kuwa nilikuwa pombe na muda huo nikihofia kama utafika salama basi nikaipokea ile namba bila kuiangalia.
Basi kwenye simu ilikuwa ni sauti laini ya binti mmoja akaidai kaichukua namba yangu pale bar na kanipenda hivyo tuongee na yuko nje ya hotel niende nitakuta kavaa high heels, top ya pink na jeans nyeusi na miwani ya jua.
Nikatoka na kufika nje kweli nikaona sehemu ya maengesho ya magari binti huyo yupo pale..kwa kuwa nilikuwa pombe basi nikawa na ujasiri na kumfuata na kisha nikaanza kumhoji maswali mawili matatu kuwa alikuwa ananinitia nini na hajui kama mimi mme wa mtu?
Yule binti akawa kama hanielewi na naongea maneno makali, ile nataka kuanza kumchapa kelebu kadhaa, akatokea kidume mmoja na sijui anabeba vyuma vyaa aina gani kwani nilipigwa braza na nashukuru mungu kanibariki mbio na yule masta wangu aliyenipa mbinu mbili ya kukwepa na ya kukimbia bila hivyo kaka kifo nilikuwa nakipigia denge.
Baada ya kufanikiwa kuchoropoka pale nafika hapa nyumbani kuicheki ile namba kumbe ni ya CHAMDOLI, kweli huyu chamdoli anautamani uhai wangu, kaka ungekuwepo pale ungelia kwa kunionea huruma"... alimalia kusema mwakibubu
Nilipokea habari hiyo kusikitisha kwa kicheko kikubwa sana na kumwambia kaka hata mimi yaliyonikuta ni siri yangu nitakusimulia tu siku ila kwa leo kama ukinitazama vyema utakuwa na majibu kisha nikamwonesha baadhi ya matuta mgongoni mwangu laiyosababishwa na ule mwiko.
Tulikaa kwa dakika kadhaa kukijadili na kutathmini juu ya azimio hili la kwanza unywaji wa pombe kupita kiasi na kisha tukagundua kuwa ulevi ni noma na kukubaliana kuachana na azimio hilo la kwanza kwani pombe zingetuua na sio azimio la kulichekea kabisa..
Tukiwa tunafikiria azimio la pili mara simu zetu zote ziliita kwa pamoja tena namba ngeni hivyo tukawa tukizitazama tu na ghafla mlango ukagongwa kwa fujo. kwa kuwa mwakibubu alikuwa hayuko poa nikasimama na kwenda mlangoni.
Ile naufungu ule mlango nilichokutana nacho.....................
Je mlango uligongwa na nani na ni nini alikutana nacho baba pachu?
Usikose kisa hiki kesho jioni
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu kwa udhamini wa Gracious HOUSE of CAKES watengenezaji maarufu na waliobobea wa keki za aina mbalimbali kwa hafla mbalimbali waliopo jijini Mbeya na wanapatikana kwa namba 0767218014
Nawe waweza kuwa mdhamini wa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo
share, like na comment
0 comments:
Post a Comment