Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Thursday, September 18, 2014

AMRI KUMI ZA FACEBOOK

AMRI YA 1
Usi-comment kwenye status ama picha iliyowekwa mwezi uliopita. Kufanya hivyo ni kuonesha unafuatilia maisha ya mtu kimya kimya.

AMRI YA 2
Usi-like picha 3 mfululizo kwenye wall ya mtu mmoja. Ni ishara kuwa unayachunguza mambo yake kimya kimya.

AMRI YA 3
Usi-comment jambo ambalo ni nje ya topic ya post husika. Kama mtu akiposti kuhusu ng'ombe wewe usi-comment kuhusu mbuzi. Bakia kwenye hoja husika.

AMRI YA 4
Usiandike status nusu nusu. Kwa mfano; usiandike 'mwenzenu nina matatizo' Wajua fika tutakuuliza una tatizo gani. Tuokolee muda wetu kwa kuandika maelezo yaliyotosha kuwa una matatizo baada ya kufumaniwa na mwenza wako.

AMRI YA 5
Kutokana na amri ya 4, kama hupo tayri kutuambia nini kilichokusibu ni marufuku kumwambia mtu kwenye comment kuwa unamu-inbox kumweleza matatizo yako.

AMRI YA 6
Usithubutu wala kujaribu wala kudiriki kum-tag mtu picha ambayo yeye hayumo wala hajakuomba ufanye hivyo.

AMRI YA 7
Kwa wanawake, kama utaamua kupiga picha bafuni ili uipost facebook hakikisha unakumbuka kuvaa kufuli lako.

AMRI YA 8
Kwa wanaume, kama msichana ata-like ama ku-comment kwenye status ama picha yako haina maana anataka umtumie inbox.

AMRI YA 9
Kwa wanawake, kama mwanaume atakutumia friend request haina maana anakupenda ama anakusudia kukutongoza.

AMRI YA 10
Kwa wanaume, kama msichana ata-accept friend request yako, haina maana ukimtongoza atakukubalia kirahisi.

MWISHO WA AMRI
Imetupasa kuitumia facebook kwa matumizi mazuri na yenye tija. Ole wao wanaopoteza muda wao facebook kutafuta wanawake ama wanaume. Watu hao watajikuta hawajafanya lolote la maana maishani na kuanza kuwaonea gere wenzao waliofanya kweli.

Ukigombana na mpenzi wako usije kutuambia facebook kwa kuwa hata mnaposigina amri huwa hamtushirikishi.

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni