WIZARA ya afya imetoa semina elekezi kwa wanahabari kuhusiana na ugonjwa wa Ebola. Semina hiyo yenye lengo la kuijuza jamii kuhusiana na ugonjwa wa Ebola, imefanyika katika Hoteli ya New Africa, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya ugonjwa wa Ebola haujaingia nchini, na juhudi zinafanyika za kuhakikisha hauingii kwa kuweka vifaa na huduma katika viwanja vya ndege, mipaka na sehemu zingine zenye kuruhusu muingiliano wa watu wa mataifa mengine.
0 comments:
Post a Comment