Duniani kuna tafiti nyingi na mara nyingi wataalamu wa masuala mabalimbali
huja na tafiti tofauti tofauti...
Moja ya tafiti ambayo imenivutia kiasi cha kuja hapa jamvini ni utofauti wa
ufundi wa jikoni baina ya mwanamke kimbaumbau na yule mwenye neema za
allah "curvaceous" ...
Inaaminika kwamba manawake wenye nyama za nyongeza 'curvy girls' wana
ujuzi mkubwa wa mapishi kuwazidi wale ambao miili yao ni vimbaumbau...
Sababu kubwa haswa inayopelekea kuwepo kwa dhana hii ni kutokana na
utofauti wa tabia za ulaji baina ya mwanamke tipwatipwa na kimbaumbau...
Wataalamu wanadai eti kwa kuwa wanawake vimbaumbau ni wavivu sana
kula basi hata ujuzi wao wa kuandaa madikodiko, mahanjumati na
mazagazaga ni mdogo pia...(hawa nafikiri ndio wale wanaochemsha nazi bila
hata kuikuna)...
Hivyo wito wangu kwetu vidume haswa wale mnaotafuta waifu matirio, kama
wewe ni mtu wa kuchunuku zagazaga hebu konsida basi hiki kigezo
usijekuwa walazwa na njaa au kutwa washinda kwa mama muuza...
0 comments:
Post a Comment