Muigizaji wa the "Expendables 3" Sylvester Stallone amekuwa mmoja wa mastaa wa Hollywood ambao wamekuwa ni waathirika wa kuzushiwa kifo. Tetesi zilizosambaa kama moto unaounguza pori/ msitu hasa hasa kupitia mitandao ya kijamii, zilianzia kupitia ukurasa feki wa facebook.
Habari hii ambayo inaonekana kusababisha panic kubwa kwa mashabiki wa muigizaji "Rambo" imepelekea kutumwa kwa salamu za huzuni kutoka kwa mashabiki wake mbalimbali kupitia mtandao wa twitter.
Hii sio maara ya kwanza kwa muigizaji huyo kuuliwa na internet, mwanzoni uvumi mkubwa wa kifo chake ulioripotiwa na Global Associate News zilidai kuwa Rambo alifariki kwa ajali iliyotokana na snowboarding.
0 comments:
Post a Comment