1. Matumizi yaliyopitiliza - Matumizi yasiyo na mipaka katika mapato yako ya mwezi sio njia sahihi ya kukupa utajiri.
2. Kutokuweka akiba ya kutosha - Kujiwekea akiba ni jambo la msingi kwa mtu yoyote yule mwenye ndoto za kuja kuwa mtu mwenye utajiri wa kutosha.
3. Kuwa na madeni yaliyopitiliza - Kuwa na madeni yasiyo ya lazima ni hatari kwa mafanikio yako kipesa.
4. Kutokuwa na plan - kushindwa kuwa na plan katika maisha ni ku plan kushindwa.
5. Kutokuwa na akiba ya dharula- Maisha ni kujiandaa kama hutakuwa na akiba ya dharula tegemea kujikuta ukiwa katika matatizo kila mara kwa kushindwa kujinasua katika baadhi ya majanga.
6. Kuanza kwa kuchelewa - Jambo gumu ni katika mbio za kuwa ba maisha mazuri ni kuja kuona ulichelewa kuanza kuweka akiba wakati ukiwa na nguvu
7. Wewe ni mtu wa lawama kuliko utendaji- Jaribu kuwa mtu wa kutimiza majukumu yako kwa muda muafaka kuliko kuwa mtu wa kulaumu na kutupia lawama kwa wenzako.Anza kufanya majukumu kwa muda muafaka sasa.
8. Unaishi leo na kusahau kuwa kuna kesho - Kuishi kwa anasa bila kuwa na adabu ya matumizi kutapelekea kuishi kwa madeni
9. Kuwekeza fedha na nguvu zako kwenye mradi mmoja haishauriki kwani unakuwa katika risk kubwa ya kupiteza vyote bila kuwa na plan B
10. Hakuna mtu atakayeweza kujua nini kitatokea au kutotokea hivyo fanya tale unayoyamudu.
0 comments:
Post a Comment