Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Monday, August 25, 2014

NDOA YA SAUDA MWILIMA SASA NI SHIDA!

Stori: Gladness Mallya
Oooh nooo! Miaka miwili baada ya kufunga pingu za maisha (ndoa) na mwanaume aitwaye Kauli Juma, imefichuka kwamba ndoa ya prizenta wa Star TV, Sauda Mwilima ina shida kwani haishi na mumewe, ikidaiwa kwamba kila mmoja anaishi nchi tofauti na mwenzake.
Prizenta wa Star TV, Sauda Mwilima akiwa na mume wake, Kauli Jumasiku ya harusi yao.
Kikizungumza na Ijumaa Wikienda, chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Sauda, kilisema kwamba baada ya wawili hao kufunga ndoa, Kauli aliondoka kwenda nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ alikokuwa akifanya shughuli zake kabla ya kufunga ndoa na hadi leo hajawahi kurudi Tanzania.
“Yaani baada ya Sauda kufunga ndoa, mumewe alikaa kwa miezi michache hapa Bongo, nasikia hata tendo la ndoa walifanya mara mbili tu.
“Hata alipojifungua na mtoto kufariki dunia kwa bahati mbaya, mumewe hakuwepo na hadi leo hajarudi, ukweli inauma sana ila Sauda ni mvumilivu kwani ndoa yake ni shida,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Sauda ambapo alikuwa na haya ya kusema:
Sauda Mwilima akivishwa pete na mume wake, Kauli Juma.
“Ni kweli anaishi Sauzi. Tangu tukiwa wachumba tulielewana kwamba tukioana kila mtu ataendelea kuishi anapoishi hivyo mume wangu anafanya shughuli zake nchini Afrika Kusini na huwa anakuja mara mojamoja akiwa na nafasi au akiwa likizo.
“Mimi siyo mtu wa kujionesha kwamba eti mume wangu yupo nchini hivyo akija huwa ni kimyakimya anakaa tunaendelea na mambo ya familia yetu basi muda ukiisha anaondoka na tulikubaliana tangu tukiwa wachumba hivyo ikitokea mmoja wetu ameamua kumfuata mwenzake na kwenda kuishi naye hakuna shida,” alisema Sauda.Sauda aliongeza kwamba ndoa yake iko vizuri na hawajaachana na endapo ingekuwa haipo asingevaa pete ya ndoa.
“Ndoa yangu haijavunjika, tuko vizuri na mume wangu japokuwa tuko mbali lakini kila mmoja anamwamini mwenzake,” alisema Sauda.
Wadau wanaifananisha ndoa hiyo na ya Aunt Ezekiel na kudai kuwa wawili hao hawachekani.

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni