Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Friday, August 22, 2014

Naamini wengi wetu tunajua kwamba, kujinyima, kufanya mazoezi, kutumia vidonge vya kupunguza uzito na mbinu mbalimbali za kupunguza uzito wakati mwingine hushindwa kufanya kazi kama inavyotarajiwa.

Hivi sasa imethibitika kwamba kutoka nje ya ndoa kwa wanandoa husababisha kupungua uzito.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtandao wa UndercoverLovers.com, umebaini kwamba wanaume wanaozisaliti ndoa zao hupungua uzito kwa wastani wa Paundi 6, wakati wanawake hupungua kwa wastani wa Paundi 10.

Utafiti huo hauwashawishi wanandoa kusaliti ndoa zao ili kupunguza uzito, bali unakumbusha ni kitu gani hutokea katika miili yetu pale tunapozisaliti ndoa zetu. Watafiti hao wamebainisha kwamba, msongo na kuhemkwa kunakotokana na kitendo cha kusaliti ndoa, huzalisha homoni ambazo husababisha kupungua uzito kwa yule anayesaliti ndoa.

“Mwanandoa anayeisaliti ndoa yake huwa anazalisha adrenaline na homoni za msongeko aina ya cortisol, mapigo ya moyo yanaenda juu na kupumua kwa kasi na kusababisha kupanda kwa msukumo wa damu na hivyo kiwango chaserotonin kinaongezeka na kuunguza calories.” Alisema Craig Jackson Profesa wa Saikoloji kutoka katika chuo kikuu cha Birmingham City. 

Hata hivyo awali katika utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha Florence ulibaini kwamba wanaume wanaozisaliti ndoa zao wako kwenye hatari ya kupata shinikizo la damu na kupoteza maisha. 

Haiyumkini vile vifo vya wanaume wanaozisaliti ndoa zao vinavyotokea katika nyumba za wageni vinatokana na shinikizo la damu kama utafiti huo wa chuo kikuu cha Florence ulivyobainisha.

Naomba Mwenyezi Mungu aniepushe na mabinti wa humu FB, nisije fia kifuani mwa mwanamke kwa kumsaliti mamaaa

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni