Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Cecilia Hamis (pichani), mkazi
wa Majoe Mjimpya Relini jijini Dar es Salaam amemlalamikia mumewe
aliyemtaja kwa jina la Hamis Juma kwamba ametembea na mbwa wao
mweusi hadi kumpa mimba.
Akizungumza na Uwazi mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwake,
mwanamke huyo alisema alibaini hilo wiki mbili zilizopita.
“Nililigundua hilo wiki mbili zilizopita. Nakumbuka ilikuwa usiku nikiwa
nimelala, nikamsikia mbwa mmoja (kati ya wawili) analia. Niliamka kwenda
kuangalia ili kujua sababu, kufika nikawasha tochi ya simu, nilishangaa sana
kumwona mume wangu yuko naye anafanya mapenzi.
“Nilimuuliza anachokifanya, akasema anammalizia shida zake kwa kuwa
hakuna mbwa wa kiume wa kumsaidia,” alisema mwanamke huyo.
Akiendelea kumlalamikia mume wake kwa madai hayo mazito, mama huyo
alisema:
“Siku iliyofuata usiku tena, nikiwa nimelala nilimsikia mbwa akilia, nikaamka.
Safari hii niliambatana na watoto wangu, tukaenda nje, kufika tukamshuhudia
mume wangu akifanya tukio kama la jana yake, nilipomuuliza akanipa majibu
yaleyale kwamba anammaliza shida zake mbwa huyo.”
Akaendelea: “Hawa mbwa waliletwa wawili wakiwa wadogo kabisa na wote ni
majike na tangu walipoletwa sijawahi kumwona mbwa dume hata siku moja
kwani mara nyingi tunawafungia kwenye banda lao.
“Na tangu mume wangu aanze mchezo huo huyo mbwa mmoja mweusi
(pichani) amenawiri kupita kiasi, naamini amempa mimba.”
Mwanamke huyo alisema kutokana na kukithiri kwa tabia hiyo, aliamua
kuwaeleza majirani ambao nao walimshauri aende kuripoti kwa mjumbe wa
eneo hilo.
Akizungumza na Uwazi, Mjumbe wa Shina Na. 26, Majoe Mjimpya, Mbaruka
Nyamaishwa alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa mwanamke huyo
akamshauri kuyapeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Stakishari.
Habari zaidi zinawekwa wazi kwamba, majirani nao walipoona mwanamke
huyo anachelewa kwenda polisi, wao walimsomba na kwenda naye ambapo
walitoa taarifa katika Dawati la Jinsia.
Mkuu wa dawati hilo, Koplo Golbert aliongozana na walalamikaji hao hadi
nyumbani kwa mdaiwa ambapo alimkagua mbwa huyo na kuwaamuru
wanandoa hao kuripoti kwenye kituo hicho cha polisi bila kukosa jana
Jumatatu saa 3 kuonana na mkuu huyo na uchunguzi kuendelea.
Uwazi lilimuuliza swali moja mwanamke huyo, ni kwa nini anasema aliamka na
kutoka nje usiku bila kueleza mumewe anakuwa wapi muda huo kwani
hakuonyesha kushangaa kutomwona kitandani?
Anajibu: “Tulitengana vyumba kwa sababu ya ugomvi wa kifamilia.”
Uwazi lilimgeukia mume wa mwanamke huyo na kumuuliza kuhusu madai
mazito ya mkewe ambapo alisema:
“Mimi sijawahi kufanya kitendo hicho na mbwa ila nahisi mke wangu na hawa
majirani wa hapa wananitengenezea hilo tukio ili nikafungwe jela maisha,
halafu wao waweze kuchukuwa mashamba yangu kwani ndani ya ndoa yangu
kumekuwa na ugomvi wa mara kwa mara.”
Uwazi lilitilia shaka uwezekano wa mbwa kunasa mimba ya binadamu, hivyo
lilimsaka daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na kumuuliza
kuhusu madai ya mwanamke huyo.
Msikie: “Mh! Binadamu kumpa mimba mbwa haiwezekani. Binadamu anaweza
kumpa mimba sokwe, kwa mbali sana nyani. Lakini si mbwa.
“Ila kama huyo mama anasema hivyo, mbwa akapimwe na ikibainika ni kweli
basi yatakuwa maajabu ya dunia maana dunia ina mambo yake.
Chanzo:udakuspecially
0 comments:
Post a Comment