Jamaa mmoja alitoka Mbeya na kwenda Tanga kutafuta maisha, kufika kule akapata bahati ya kuwa meneja katika kiwanda kimoja maarufu pale jijini.
Kijana huyu alikuwa ni mtu wa kujirusha sana na alikuwa akiamini ya kuwa hakuna furaha zaidi ya kula bata akiwa bado mzima na meno yangali yapo.
Siku moja akiwa club majira ya usiku akakutana na demu mmoja wa ukweli sana (chotara) na kucheza nae huku akimtupia maneno jamii ya ndoano ili aweze kumnasa yule manzi.
Muda wa kuondoka wakaondoka wote na kwa kuwa anakaa karibu na ule ukumbi hakuchukua cab akatembea uchochoroni na kufika home na kisha akajisevia ule mzigo.
Asubuhi akashangaa kuamka na kushuhudia yule manzi hayupo pale akaenda bafuni na sehemu zote akaona hakuna dalili ya yule binti basi akaamua alale zake hasa ukizingatia ilikuwa ni mapumziko ya kusherehekea siku ya uhuru.
Zikapita siku kadha siku moja akiwa anarudi home majira ya saa nne usiku akakutana na yule dada uchochoroni na kumwambia kuwa alikuwa anamsubiria jamaa, na chakushangaza kabisa yule binti akamwita jamaa kwa jina halisi wakati yeye alimtajia jina feki kama haya tuyatumiayo hapa facebook.
Wakaongea pale na jamaa akamvutia home na mambo yakaendelea kama kawaida yao na baada ya kukaa kwa muda mrefu jamaa akamwomba demu aende kuwaona wazazi wake na kujitambulisha ili wajue wana mkwe wao mtarajiwa.
Baada ya mvutano wa siku kadha demu akiwa anakataa hatimaye akakubali waende zao na kumwahidi atamfuta siku ya pili na wakutane hotel moja karibu na ufukwe wa bahari ya hindi.Jamaa akauliza sasa kwa nini twende jioni si tutachelewa kwani ni wapi?
Demu akamwambia usijali kabisa yaani.
Siku ya pili jioni jamaa akafika pale hotelini wakakaa karibu na ufukwe wakipiga story na kisha giza lilipotanda akamchukua jamaa na wakawa wanaifuata bahari na walipoanza kugusa maji binti akamwambia jamaa apande mgongoni mwake na afunge macho asifungue mpaka atakapo mwambia afumbue.
Baada ya kumbwambia afumbue wakawa wako kwenye mji mmoja wenye watu weupe jamii ya watu wenye asili ya bara Asia na kuna mtu akaja naongea kiswahili bomba na kuwaambia wavue zile nguo walizotoka nazo duniani na kupewa nguo za hariri ambazo ndio zavaliwa huko.
Baaada ya kuvaa akapewa chumba na muda mfupi baadae akaitwa na wazazi ambao wao wakaanza kumsimulia jamaa maisha yake kutoka akiwa mbeya mpaka pale tanga na kumwambia kwamba wamekubali amwoe mtoto wao ila kwa masharti ya kutofanya kazi na kuishi nae kwani hela wao watawapa.
Akwa anashangaa anataka kujua hizo hela zitakuwa na malipo? basi baba akamwambia kijana mmoja ampeleke store yule mkwe na kumwonyesha fedha za mataifa mbalimbali zikiwa kwenye kile chumba.
Basi jamaa akakaa pale kwa siku tatu, ile siku ya mwisho akaambiwa sasa atarudi kazini, ingawa ametafutwa kwa muda na bosi bila kuonekana atapewa barua ya kuachiswa kazi yeye aichukue bila hofu na baada ya siku ya tatu ataitwa arudi kazini na kuongezewa marupu rupu ila yeye akatae.
Basi kijana siku ya pili asubuhi akajikuta yuko home kitandani na wakati anafikiri anaota yule binti kaja na kusema yeye anarudi kwa wazazi hivyo atakaa kidogo kule kisha atarudi tena baada ya siku kadha na kumwambia jiandae usije chelewa kazini.
Kijana akaenda kazini na kupata barua ya kuachishwa kazi na siku ya tatu akaitwa na kagoma na yule binti akawa sasa karudi. Wakakaa mwaka mmoja na kuzaa mtoto mmoja na kisha kijana akamwambia anataka x-mass waende mbeya wakasalimie.
Wakati wako kwenye basi kwenda mbeya kila wakikaribia sehemu ya kupata chakula binti anatoweka kwenye gari na wakikaribia kituoni binti basi likisimama anakuja akiwa na chakula tayari.
Jamaa akawa anashangaa ila hana cha kuuliza, walipofika mbeya binti akagoma kabisa kuonana na wazazi wazazi wa yule kaka akitaka abaki hotelini na baada ya kulazimishwa mama yeye akasema lazima tumwone aliyekuzalia mtoto bomba kama huyu.
baada ya mama kuja na kumwona yule binti siku ya pili yake akafa huku binti akigaramia kila kitu na baada ya msiba kwisha wakarudi tanga na wakiwa njiani wakapata ajali ya basi kaka na mtoto wakapona ila dada yule mpaka leo hajulikani kama alitowekaje maana mpaka sasa ni mwaka wa saba hajatokea na wala hakuna dalili na mtoto yule sasa yupo darasa la kwanza na kaka anaogopa kuoa kwani hajui nini kitatokea binti akirudi kama kawaida yake bila taarifa.
Tafadhali hakuna ukweli wowote hapa nina njaa tuu na chakula naona chachelewa hivyo nakikakosa cha kufanya na kutunga huu upuuzi.
kama wewe sio mpuuzi share na kommenti "hujanipata"
0 comments:
Post a Comment