IMEVUJA kwamba Staa wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ndiye aliyemshauri Nasibu Abdul ‘Diamond’ asioe kwa sasa ili asishuke kimuziki.
Ushauri huo umekuwa mwiba kwa mpenzi wa Diamond, Wema Sepetu ambaye amekuwa na ndoto ya kuolewa na staa huyo anayekimbiza kitaani na wimbo wake wa Mdogomdogo.
Akifafanua zaidi kuhusiana na ushauri huo, Nay alisema: “Kuna mifano mingi sana nimeiona kutoka kwa wasanii ambao wameoa, wengi wao wameshasanda sasa mdogo wangu (Diamond) na yeye alipoleta hoja ya kutaka kuoa nikaona sasa anatafuta shimo la kwenda kujifukia, nikamshauri aache.”
CREDIT : GPL
0 comments:
Post a Comment