Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Friday, August 15, 2014



Yule zilipendwa wa sexy lady wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper
Massawe aitwaye Ramadhan Abdallah Mtoro ‘Dallas’ anadaiwa kukumbuka
shuka kukiwa kumeshakucha ikielezwa kwamba eti anabembeleza kurudiana
na staa huyo waliyetengana takriban mwaka mmoja uliopita ili wakamilishe
taratibu za kufunga pingu za masha.

Akizungumza na Amani hivi karibuni kwenye Ukumbi wa Lango la Jiji uliopo
Magomeni, Dar, Dallas alisema kuwa anamshangaa Wolper kumkatalia ombi
lake la kurudisha uhusiano wao wa kimapenzi huku akijua fika kuwa bado
anampenda. “Nampenda sana Wolper. Pliz namuomba turudiane tu.

Ningejua kipindi kile nilivyorudi kutoka nje ningefunga naye ndoa kwani sasa
hivi angekuwa ni mke wangu niliyechaguliwa na Mungu lakini ndiyo hataki,”
alisema Dallas. Kwa upande wa Wolper alisema kuwa Dallas kwa sasa ni
mshikaji wake tu na atabaki kuwa hivyo lakini kuhusiana na mapenzi, hakuna
kitu kama hicho

“Nitasaidiana naye kwa kitu kingine lakini siyo mapenzi, kwa sasa niko na
mtu wangu,” alisema Wolper. Kabla ya jahazi kwenda mrama, penzi la Wolper
na Dallas lilitikisa mji huku kukiwa na maneno mengi ambayo yalimshinda
mkali huyo wa filamu za Kibongo ambaye aliamua kuchukua hamsini zake


0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni