Facebook
Twitter

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "

SOMA HADITHI KALI NA YA KUSISIMUA "SIMU YA AJABU "
Fuatilia kisa hiki kila siku jioni kupitia ukurasa wa Simu ya Ajabu. Nawe waweza kutumiwa kisa hiki cha kusisimua kinachosomwa na wengi kupitia whatsapp namba 0713317171 au kuipiga namba hiyo

Wednesday, August 6, 2014


Staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson anadaiwa kukinukisha
nyumbani kwa Wema Isaac Sepetu baada ya kunusurika kufumaniwa na
mume wa mtu, Moses Peter Iyobo a.k.a Moze Iyobo ambaye ni densa wa
Nasibu Abdul ‘Diamond’.

Habari zisizokuwa na shaka zinadai kwamba tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita
nyumbani kwa Wema, Kijitonyama, Dar ambapo Aunt alisababisha tafrani
iliyosababishwa na mke wa mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Mwengi
Ally.

Kwa mujibu wa mashuhuda wetu waliokuwa wakizungumza kwa kupokezana,
Mwengi alidai kwamba Aunt amekuwa akitembea na mumewe huyo hivyo
timbwili lilianzia nyumbani kwa Aunt, Mwananyamala A jijini Dar.

Ilidaiwa kwamba, huku Aunt akiwa hajui hili wala lile, ghafla waliibuka wasichana saba na kumuanzishia mwigizaji huyo.Mashuhuda hao walidadavua kwamba katika kujinusuru na kipigo ambacho alihisi akiwa peke yake, angeumizwa Aunt alikimbilia nyumbani kwa shoga yake, Wema.

Ilidaiwa kwamba wasichana hao hawakuishia hapo kwani walimkimbiza Aunt
hadi wakamuona akiingia kwa Wema ambapo walipofika getini walikutana na
meneja wa msanii wa Bongo Fleva, aitwaye Mirrow, Petit Man ambaye
walimuomba amtoe Aunt ili wamshikishe adabu ajifunze kukaa mbali na
waume za watu.

Ilisemekana kwamba katika tafrani hiyo getini, Wema alitoka na msichana
wake aitwaye Careen lakini Aunt hakutoka ambapo waliwaambia wasichana
hao kuwa Aunt hawezi kutoka na isitoshe wa kulaumiwa ni Moze Iyobo kwani
yeye ndiye anayedaiwa kumtongoza Aunt na kuanza kuchati naye hadi
mkewe akanasa meseji zao za mapenzi.

Baada ya kujazwa data hizo, Mwandishi alimtafuta Mwengi ili kupata maelezo
ya kina kuhusiana na ishu hiyo ambapo alikiri kwenda kwa Aunt na Wema
lakini hakufanikiwa kumpata Aunt kwani kama angemkamata, maafa
yangetokea.Mwengi alisema kuwa siku ya tukio aliitwa na Aunt maeneo ya
Mlimani City, Dar na akamwambia aende na mtoto akamfanyie shopping.

Alisema baada ya kuambiwa hivyo hakuwa na hiyana kwani alijua kuwa ni
kama mama yake mkubwa na shoga wa mpenzi wa baba yake mkubwa
ambaye ni Diamond, kumbe nyuma ya pazia kulikuwa kuna kitu kingine
kimejificha.“Niliporudi nyumbani, mume wangu aliniambia nimpige picha kwa
kutumia simu yake, nilipoifungua ndipo ikaingia meseji kutoka kwa Aunt.

“Nilipoisoma ile meseji nikagundua kuwa walianza kuchati muda mrefu
kuhusu mapenzi yao, ndipo nikakusanya jeshi langu na kumfuata nyumbani
kwake nikamshikishe adabu, amshukuru Wema kumficha maana sipati picha
kwa jambo ambalo lingetokea. Ingekuwa mwisho wake wa kupora waume za
watu,” alisema Mwengi.

Alipotafutwa Aunt na kuulizwa juu ya sakata hilo, alijibu kwa kifupi: “Sina
muda mchafu wa kuongea halafu nimelala, kwa sasa niache nipumzike.”

crdt: Udakuspecially

0 comments:

Post a Comment


  • Copyright 2014 Uvunguni