1.Usiwe mtu wa kulalamika kwa sababu hakuna mtu liye sahihi sana katika maisha haya.
2. Usimlaumu mtu hapa duniani kwani ulizaliwa peke yako na kila jukumu mbele yako ni lako wewe na utakufa peke yako.
3. Usijaribu kulazimisha watu wafikiri kama wewe au kuwahukumu watu kwa jinsi unavyofikiria wewe, jitahidi kuwa upande wa pili wa wao kabla ya maamuzi
4. Usiwe mtu wa kunung’unika kila wakati kwani hiyo hukupunguzia mori na ari ya kazi
5. Usijimilikishe mambo na majukumu makubwa ukidhani utaishi milele kuwa na kiasi nacho hakitapotea….
6. Usijisifie na kujipa ufahari mapema kumbuka bado tupo safarini na kunaweza kutokea lolote njiani
7. Usiwe na wivu mbaya kwani kila kitu ni matokeo ya mtu kujituma na Mungu kukamilishia mipango yake kwako.
8. Kamwe usitengeneze nafasi ya kisasi katika moyo wako kwani malipo yake huangamiza nafsi na moyo wako pia
9. Usijaribu kwa namna yoyote kumsababisha mtu akakosa riziki yake na familia yake kwa makusudi au bahati mbaya, dhambi hiyo huwa na doa lisilofutika na hukuandama kama laana
10. Kuwa mwepesi wa shukrani kwa kila jambo jema kwako hata kama ni dogo kiasi gani
11. Daima epuka: Unafiki, Umbea na majungu bali wewe kuwe mwenye busara kwa kila jambo
12.Tabasamu na kumtakia rafiki yako siku njema
Dunia imejaa visa na mikasa ambayo kila mtu hukutana nayo kwa nafasi yake. Lakini wakati wewe unafikiri ya kuwa umeumia au kuumizwa zaidi wapo ambao wao wanapitia makubwa zaidi yako.
Kuna watu wao baada ya kupitia mapito haya hukata tamaa ila kuna ambao wao hupigana mpaka tone la mwisho kuhakikisha wanakabiliana na changamoto hizo.
Kuna wale ambao hudhania umaskini ndio sababu kubwa ya kuwafanya wawe makatili hasa wakiangalia wapi walikopitia, lakini pia kuna wale ambao kutokana na mali na utajiri wao huamua kutumia fedha hizo kulipa visasi au hata kuhatarisha maisha ya wenzao.
Kutana na SAMIRA katika simulizi hii na ujifunze mengi.
Hapo chini kuna link za simulizi hii kuanzia namba moja mpaka ilipofikia sasa, na kuanzia leo ukiikosa hapa basi utaikuta kupitia karibumbeya.com
Soma Sehemu ya 2
Soma Sehemu ya 5
Soma Sehemu ya 7
Soma Sehemu ya 9
Soma visa vingine HAPA